24 Machi 2016 - 18:49
 Shein aapishwa kuwa rais wa Zanzibar

Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, ambaye amejipatia ushindi kiurahisi baada ya chama pinzani kususia Uchaguzi ameapishwa kuwa rais.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, ambaye amejipatia ushindi kiurahisi baada ya chama pinzani kususia Uchaguzi ameapishwa kuwa rais.

Ali Mohamed Shein wa visiwa vya Zanzibar nchini Tanzania leo ameapishwa kwa kipindi kengine cha miaka tano madarakani baada ya kutangazwa mshindi wa marudio ya uchaguzi uliofanyika tarehe 20 Machi. Shein aliapishwa katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar na kuhudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania John Pombe  Magufuli na marais wastaafu Ali Hassan Mwinyi na Amaan Abeid Karume. Katika hotuba yake ya kuapishwa rais Shein ameahidi kuwaunganisha wanzanzibari na kudumisha muungano na Tanganyika. Marudio ya uchaguzi huo wa Jumapili yamefanyika baada ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ZEC kufuta uchaguzi wa awali wa tarehe 20 Oktoba kwa madai ya udanganyifu. Wanadiplomasia 15 wa Ulaya na Marekani wametowa taarifa ya pamoja kusikitikia kitendo cha marudio ya uchaguzi huo uliosusiwa na chama kikuu cha upinzani cha CUF.

Wachambuzi wa siasa wengi wanaona kuwa Marudio haya ya Uchaguzi ni dosari kubwa kwa serikali ya Zanzibar na Tanzania kwa Ujumla.

Mwisho wa habari/ 291